0
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewataka wamiliki wa daladala ambao watahitaji vyombo vyao kutumia barabara ya Kambarage iliyopo Mwenge jijini Dar es salaam wajitokeze ili wapatiwe leseni kwa ajili ya mabasi hayo kuanza kupita rasmi katika barabara hiyo.

Channel Ten imezungumza na mkurugenzi wa udhibiti usafiri wa barabara ni Sumatra Johansen Kahatano ili kujua hatua iliyofikiwa kuhusu kutumika kwa barabara hiyo ya Kambarage ambapo amesema Sumatra imepokea maombi ya wasafirishaji abiria mjini wawili ambao wanataka kupitisha daladala zao katika barabara hiyo.

Bwana Kahatano amewaomba wamiliki wengine wa mabasi ya daladala ambao watahitaji kutumia barabara hiyo kuwasilisha maombi kwani fursa bado ipo.
Aidha amesema kamati ambayo iliteuliwa kushughulikia uboreshaji wa barabara hiyo bado inaendelea ili kuwezesha wananchi kupata usafiri kwa karibu zaidi.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga wamezungumzia barabara hiyo .

Post a Comment

 
Top