Hii imezoeleka mpambano kati ya timu hasimu za Simba na Yanga
zinapokutana kunakuwa na vitendo vya kishirikina vinakuwa vinafanywa
uwanjani lakini kwenye mechi ya jana baina ya timu hizo visiwani
Zanzibar hakukuwepo na vitendo hivyo.
Unajua ilikuaje soma hapa: uwanjawa Amaan ulipofanyika mchezo huo
umekuwa ukitumiwa na jeshi la Zanzibar kwa ajili ya kufanyia mazoezi
kuanzia asubuhi hadi majira ya alasiri kwa ajili ya kujiandaa na sherehe
za Mapinduzi ambazo zitafanyika kesho Alhamisi.
Pale uwanjani walishuhudiwa makomandoo wa timu hizo wakiwa wanahaha
kuzama ndani na kufanya mambo yao lakini wanajeshi waliokuwa wanafanya
mazoezi uwanjani hapo hawakuruhusu mtu yeyote asiye mwana usalama
kuingia ndani ya uwanja huo hadi saa tisa walipoziruhusu timu za Taifa
ya Jang’ombe na Azam.
Kutokana na hali hiyo makomandoo hao walilazimika kukaa nje na juhudi
zao za kutaka kufanya vitendo vya kishirikina vikakwama huku wengine
wakionekana kuwasiliana kwa simu mara kwa mara.
Post a Comment