0
Tabora.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amesema wanaendelea kuchunguza tukio hilo.

Mmoja wa watoto wa marehemu, Tatu Juma amesema walibaini mama yao kajinyonga baada ya kuwasha taa ili ampeleke mdogo wake kujisaidia.

“Nilimsikia mdogo wangu akimwita mama ampeleke chooni bila mafanikio, ndipo nilipowasha taa na kumwona mama amening’inia darini,” amesema Tatu.

 Akizungumzia tukio hilo, mume wa marehemu, Juma Kiligito amesema siku hiyo alilala kwenye nyumba ya mke mkubwa ndipo alipoamshwa na mtoto wake Tatu akimweleza mama yao amejinyonga.

“Hatujawahi kuwa na ugomvi wala tofauti yoyote kabla ya tukio hili. Hata usiku alipojinyonga tulikula na kuzungumza kwa pamoja kabla ya kila mwanamke (wake zake) kutawanyika kuingia chumbani kulala,” amesema Kiligito.

Katika tukio jingine, mkazi wa Kijiji cha Nyarututu Wilaya ya Chato mkoani Geita, Anastazia Kahezi (65) amejinyonga kwa madai ya kuwa na msongo wa mawazo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wanaendelea na uchunguzi ili  kujua sababu za  Anastazia anayedaiwa pia kuwahi kuugua ugonjwa wa akili kujiua.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyarututu, Silvester Nalompa amesema Anastazia alijinyonga kwa kutumia kipande cha kanga yake.

Post a Comment

 
Top