0
dara ya uvuvi mkoa wa Geita imekamata wafanyabiashara saba wa Samaki waliokuwa na kilo kumi na moja elfu mia nane tisini na sita zenye thamani ya shilingi millioni kumi na moja mianane tisini na sita.

Wafanyabiashara hao wamekamatwa saa nane usiku katika kata ya Senga wilayani Geita ambapo gari aina ya Hiace yenye namba za usajiri T199 AUN ikiwa imepakia Samaki ambapo afisa ufawidhi ubora wa Samaki na usimamizi wa rasilimali za uvuvi Shafii Kiteri amesema watafikishwa mahakamani.

Aidha Kiteri amesema serikali kwa muda mrefu imekuwa ikitoa elimu kwa wavuvi kutovua Samaki walio chini ya nchi moja na nusu lakini wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakisafirisha samaki usiku.

Nico James ni dereva wa gari lililokamatwa likisafirisha samaki hao usiku inadaiwa kuwa amekuwa akisafirisha samaki zilizochini ya kiwango ndipo alipotegewa mtego na hatimaye kukamatwa.

Baadhi ya wafanyabiashara na wavuvi wa samaki wameiomba serikali kudhibiti nyavu zisizotakiwa kutoka kiwandani tofauti na sasa ambapo vita kubwa imeelekezwa kwa wavuvi wanaokwenda kununua madukani.

Post a Comment

 
Top