0
Vinara wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Simba watakuwa wenyeji dhidi ya Azam FC katika mwendelezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania ,mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Wawakilishi wa vilabu hivyo ambao ndio wasemaji Jaffary Idd Maganga na Hajji Manara kila mmoja ametamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu ambapo Simba watakuwa wakitaka kiurejesha matumaini kwa mashabiki wake kufuatia kufungwa katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi lililofanyika Visiwani Zanziba mwezi mwanzoni mwa mwezi huu.

Manara ametamba kuwa hawataendelea kuwa wataeja wa Azam FC kwani wamejipanga kuibuka na ushindi na kuendelea kujikita kileleni katika Ligi , wakati Jaffary Idd amesisitza kuendelea ubabe kwa vigogo hao wa Ligi kwa kuwafunga.

Post a Comment

 
Top