0
Huko Mkoani Kilimanjaro, Jeshi la polisi limewatoa hofu askari walioathirika na tukio la ajali ya moto uliotokea juzi usiku kwenye makazi ya askari hao yaliyopo katika manispaa ya Moshi na kuteketeza vyumba 9 pamoja na malizote zilizokuwa ndani ya vyumba hivyo vyenye thamani ya zaidi ya sh 93 mil/=

Akizungumza kwaniamba ya Inspekta jenerali wa polisi baada ya kutembelea eneo la tukio kamishna wa polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo Cp Marijani Sato amesema licha jeshi hilo kuahidi kuwasaidia askari hao pia limetoa fursa kwa waathirika kuchagua maeneo mengine ambayo wangependa kufanyi a kazi.

Awali akisoma taarifa ya tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbrod Mutafungwa amesema moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana ulithibitiwa baada ya wananchi kwa kushirikiana na vikosi mbalimbali vya zimamoto kutoka manispaa ya moshi,tpc na uwanja wa ndege wa kia.

Hii ni mara ya pili kuzuka kwa moto kwenye jengo hilo lenye ghrofa mbili,ambapo kwa mara ya kwanza n i mwaka 2008 na mara ya pili tarehe 25 mwezi huu,ambao licha ya kutoleta madahara kwa wanadamu uliteketeza malizote za familia 9,ambazo kwa zimepatiw ahifadhi ,kwenye chuo cha taaluma ya polisi Moshi.

Post a Comment

 
Top