0
Dar es Salaam. Wafanyakazi wa kampuni za simu na zile zinazojihusisha na huduma kwa wateja zinazohusiana na mawasiliano ya simu, huenda wakapoteza ajira, ikiwa ni mkakati wa kukuza kampuni au kukabiliana na hali ya kibiashara.

Katika taarifa tofauti, Vodacom imesema inataka kufanya mageuzi ya kiutendaji yatakayoiwezesha kukua zaidi. ISO BPO, ambayo ni wakala wa ajira wa kampuni za simu, imeeleza inataka kupunguza wafanyakazi kutokana na biashara yake na Tigo na Airtel kupungua.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Vodacom, Ian Ferrao inasema lengo la kupunguza wafanyakazi ni kuifanya Vodacom kuwa na mfumo wa uendeshaji fanisi utakaoendana na  mabadiliko ya kasi sokoni.

Katika taarifa nyingine iliyotolewa na Tigo, inaeleza kuwa mkataba wa kutoa huduma kwa wateja kwa niaba ya Tigo unaisha Januari 31, hivyo wafanyakazi ambao walikuwa kitengo hicho watapoteza ajira.

Hata hivyo, meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa kampuni ya ISON BPO ndiyo inatakiwa kutoa maelezo kuhusu mchakato huo kwa sababu si waajiriwa wa Airtel.

Post a Comment

 
Top