0
Mbeya.  Msichana wa kazi za ndani, Fidea Lucas (30) aliyemwagiwa tindikali, jana alimwelezea Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya,  Amos Makalla namna alivyofanyiwa unyama huo.

Akiwa amejifunika mtandio usoni, Fidea alieleza jinsi alivyomwagiwa tindikali na mfanyakazi wa duka la mwajiri wake ambaye ni mfanyabiashara.

Alisema alikuwa akifanya kazi za ndani nyumbani kwa mfanyabiashara huyo jijini Mbeya na baada ya kuanza kumdai stahiki zake za miaka tisa, alimbadilisha kitengo cha kazi na kumpeleka Makongorosi kuuza duka na  siku chache alimwagiwa tindikali na mfanyakazi mwenzie.

“Baada ya kumwagiwa tindikali, tulikamatwa wote wawili na kupelekwa mahabusu, lakini jambo la kushangaza mwenzangu aliachiwa kwa kudhaminiwa na mwajiri wetu. Nilishikiliwa  polisi mwezi mmoja. Kila siku nilikuwa nikihamishwa kituo mara Mbeya au Chunya bila kujua kosa langu,” alisema.

Baada ya kupokea malalamiko hayo, Makalla aliwaagiza polisi kuwakamata watuhumiwa mara moja.

“Sihitaji porojo katika hili, huyo mama amenyanyasika,” alisema Makalla aliyekuwa kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika Ukumbi wa Mkapa jijini hapa.

Post a Comment

 
Top