0
Wananchi wa Mtaa wa Chalagule kata ya Mlimani wilayani Morogoro wakiwa na silaha za jadi wamewazuia watendaji wa serikali kutekeleza operesheni iliyo tangazwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro ya kuondoa na kubomoa mifereji na miundombinu ya maji ambayo imejengwa kwenye vyanzo vya maji bila kufuata taratibu za kisheria.

Wakiwa na silaha hizo za jadi wananchi hao wamepinga operesheni hiyo kwa madai kuwa haikuzingatia usawa katika matumizi ya maji na baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya wananchi na watendaji hao zoezi hilo likasitishwa.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk.Kebwe Steven Kebwe amesema opresheni hiyo ipo kisheria na ni utekelezaji wa makubaliano ya mkakati wa kukabilana na changamoto za upatikanaji wa maji ikiwemo kuwaondoa wananchi waliovamia na kufanya makazi na shughuli za kibinadamu katika milima ya uluguru.

Afisa wa bodi ya maji bonde la Wami- Ruvu Praxeda kalugendo amesema wananchi hao wamekiuka sheria kwa kujenga na kutumia maji bila kuwa na vibali.

Post a Comment

 
Top