0
Kikosi cha Yanga

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema anaamini kikosi chake kipo vizuri kwa ajili ya mchezo huo na watajituma kulingana na walivyopokea mafunzo ili kuweza kutetea Ubingwa huo.

“Wachezaji wote wapo kwenye  hali nzuri na wanamorali ya kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri katika michuano hiyo ambayo ipo  katika hatua ya tano," amesema Mwambusi.

Yanga inashuka dimbani huku ikiwakosa baadhi ya nyota wake  ambao ni Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Justin Zullu na Malimi Busungu  ambaye bado ana matatizo ya kifamilia.

Mechi nyingine zinazopigwa leo ni Alliance dhidi ya Mbao FC katika dimba la CCM Kirumba Mwanza pamoja na Majimaji wanaokutana na Mighty Elephant mjini Songea

Post a Comment

 
Top