Kikwete amefunguka hayo leo katika kipindi cha East Africa Breakfast cha
EA Radio, kinachoruka kila siku saa 11:00 alfajiri hadi saa 3:00
asubuhi.
Ametumia nafasi hiyo kuishauri serikali kuifikisha mwisho vita hiyo, ili
kulimaliza kabisa tatizo hilo kwa kuwa limepoteza vijana wengi wenye
uwezo mkubwa na mchango katika taifa, huku akitolea mfano uwezo wa
msanii wa Bongo Fleva, Langa ambaye kwa sasa ni marehemu ikidaiwa kuwa
alipoteza maisha kutokana na dawa hizo, pamoja na shida alizokuwa
akizipata msanii Ray C, za kutafuta dawa hizo hata usiku wa manane.
Ameitaka mamlaka mpya wa dawa za kulevya kuwachunguza watu 97 ambao
majina yake yamekabidhiwa hivi karibuni na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda, na yeyote atakayethibitika kuhusika, achukuliwe hatua,
huku akionesha imani kubwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Rogers
William Sianga.
Post a Comment