Msanii wa bongo movie Wastara amemchana mpenzi wake wa sasa Bond kwamba
asipojirekebisha baadhi ya tabia zake atamuacha na akimwacha hatarudi
tena kwake.
Hata hivyo Wastara amesema anaweza kuvumilia shida anazopata kwa Bond
lakini anaweza kumuacha muda wowote kwani hahitaji 'stress' za kimapenzi
huku akiweka wazi kuwa amejitahidi na amefanikiwa kumrekebisha kwa 80 %
na endapo ataendelea na mambo yake ya zamani zamani ataachana naye.
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Wastara amesema "Niseme tu ukweli kwamba
kwa Sajuki hakuna mtu anayeweza kufikia upendo wetu kwa kuwa Sajuki
alikuwa anajali kila kitu ambacho nilikuwa nakipenda, kitu ambacho mpaka
sasa sijapata ni mtu ambaye amefikia hatua za Sajuki ". Alisema
Wastara.
Post a Comment