Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva The Bosslady
amefunguka kwa kudai kuwa katika mastaa wa muziki Alikiba ndiye msanii
ambaye anatamani kudate naye.
Diva ambaye kwa sasa anatoka kimapenzi na muimbaji Heri Muziki, alikuwa
host wa show ya Valentine’s Day iliyofanyika Jumatano hii katika ukumbi
wa Next Door na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali.
Akiongea na waandishi kabla ya kwenda kusherehesha show hiyo
iliyoandaliwa na Irene Uwoya, Diva alidai Alikiba ndiye msanii ambaye
anatamani kudate naye.

“Alikiba ndiyo msanii au staa ambaye natakamani kudate naye,” Diva
alisema baada ya kuulizwa ni staa gani ambaye anatamani kudate naye.
“Sijawahi kutoka naye kimapenzi, pia sasa hivi mimi nipo kwenye
mahusiano na mtu mwingine,”
Mtangazaji huyo alidai yeye wanaume wake wengi anawapata kupitia kipindi
chake la Ala za Roho ambacho huchambua mambo mbalimbali kuhusu
mahusiano.
Post a Comment