Viongozi hao saba walifungwa Jumatatu baada ya kupatikana na hatia ya kutofuata uamuzi wa ahakama wa kumaliza mgomo wa madaktari ambao umedumu kwa miezi miwili unusu sasa.
Viongozi hao wametakiwa kuhakikisha suluhu ya mgomo huo inapatikana katika kipindi cha siku saba.
Mazungumzo ya kutafuta suluhu yataongozwa na Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) na Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNHCR).
Madaktari wamekuwa wakiitaka serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka
2013 ya kuwaongezea mishahara na kuboresha mazingira ya utendaji kazi
hospitalini Wanataka pia serikali iwekeze zaidi katika dawa, vifaa na
mitambo hospitalini pamoja na kutoa pesa zaidi za kufadhili utafiti wa
matibabu.
Wamekataa mshahara walioongezewa na serikali wa asilimia 40 wakisema kuwa ni wa chini kuliko ule walioafikiana mwaka 2013.
Karibu madaktari na wauguzi 5000 kutoka hospitali 2000 za umma, walianza
mgomo wiki ya kwanza ya mwezi Desemba na wagonjwa wamekuwa wakikosa
matibabu.
Post a Comment