0
Dodoma. Katika harakati za kutaka kujisafisha, CCM imeamua kurudi kwenye misingi ya Azimio la Arusha lililoanzishwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1967.

Azimio hilo lilifafanua falsafa ya ukombozi wa kiuchumi na kijamii chini ya misingi ya ujamaa na kujitegemea kama lengo la muda mrefu kwa Watanzania.

Jana, chama hicho kilijinasibu kuwa sasa kinaanza kuyaishi maagizo na uamuzi wa azimio hilo.

Katibu wa Nec ya CCM, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole aliliambia gazeti hili kuwa uamuzi wa kuliishi na kulienzi Azimio la Arusha ndani ya chama hicho hauna mjadala.

Polepole alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa mdahalo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ambao ulihudhuriwa na viongozi wa CCM na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba.

Moja ya jambo alilosisitiza ni la viongozi kujilimbikizia vyeo akisema hakuna atakayepona kwenye uamuzi huo, kwa kuwa walishakubaliana.

Post a Comment

 
Top