Dar es Salaam. Licha ya kuwa na matokeo ya wastani katika mtihani
wa kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni na Baraza la Mitihani la
Tanzania (Necta), shule zenye majina ya viongozi maarufu nchini
zimeendelea kuadimika kwenye 10 bora.
Katika matokeo hayo, shule 38 zenye majina ya viongozi wa kada na ngazi mbalimbali ambazo mwandishi wetu amechambua matokeo yake, hakuna hata moja ambayo imetoa wanafunzi 10 waliofaulu kwa kiwango cha Daraja la Kwanza (Division One).
Akizungumzia matokeo ya shule hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alisema hakuna uhusiano wowote wa jina la kiongozi na ufaulu au kufeli kwa shule hizo.
“Kama kuna shule yenye jina la kiongozi na imefanya vizuri matokeo haya, basi mhusika huko aliko lazima atakuwa na furaha na ataangalia namna gani ataweza kuisaidia shule husika.
“Lakini kwa shule yenye jina la kiongozi halafu imefanya vibaya, mhusika lazima ajisikie vibaya. Ningependa kuziona shule zenye majina ya viongozi zikiongeza juhudi ili wahusika wapate morali zaidi wa kuzisaidia,” alisema Simbachawene.
Alizitia shime shule zilizofanya vyema na kuwaomba wenye majina hayo kuziunga mkono kwa hatua hiyo ya maendeleo.
“Zile zilizofanya vibaya naomba tushirikiane kwa sababu mimi ndiyo msimamizi wao. Natambua kuna changamoto lakini tukiwa pamoja, tutajua namna gani ya kuzitatua,” alisema Simbachawene.

Post a Comment