Wabunge kupitia kamati yake ya miundombinu imeishauri serikali
kuzifanyia kazi kwa kina changamoto zilizopo kwenye bandari za Tanzania,
ikiwa ni pamoja na kuangalia upya wa sheria iliyoanzishwa ya kodi ya
ongezeko la thamani (VAT) kwa huduma zitolewazo na mawakala.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shuguli za kamati kwa kipindi cha januari 2016 hadi januari 2017, mwenyekiti wa kamati ya bunge ya miundombinu profesa Norman Sigalla amesema sheria hiyo inaenda kinyume na sheria za kimataifa, na hivyo kufanya wateja kutotumia bandari za Tanzania.
Aidha, wakichangia taarifa hiyo ya kamati na ile ya kamati ya Nishati na Madini, Mbunge wa Sumve Bw. Richard Ndassa akahoji ni kwa kiasi gani ushauri unaotolewa na wabunge unatekelezwa na serikali na Mbunge wa viti maalum (CHADEMA) Bibi. Jesca Kishoa akitaka serikali itekeleze sheria ya kuweka mikataba wazi.

Post a Comment