0
 Andrea Giesbrecht apatikana na hatia ya kuficha mabaki ya wototo wachanga kwenye kabati kazini.

Mwanamke huyo kutoka mji wa Winnipeg, makao makuu ya jimbo la Manitoba nchini Canada, amepatikana na hatia ya kupeleka na kuficha mabaki ya wototo sita ndani ya kabati hilo.

Andrea Giesbrecht ameshtakiwa kwa makosa sita ya kuficha miili ya wototo hao.

Kila kosa lina adhabu ya kufungwa miaka miwili jela.

Jaji wa mahakama ya jimbo la Manitoba, Murray Thompson, alisoma hukumu hiyo, baada ya kumalizika kwa kesi hiyo iliyodumu mwezi mmoja.

Mabaki ya watoto hao yalipatikana mwezi Oktoba mwaka 2014.

Jaji Thompson alisema kuwa, ushahidi uliotolewa katika kesi hiyo "umeeleza bayana" kwamba, Bi Giesbrecht alificha mimba yake na baadaye kuwazaa watoto hao sita, bila ya kujulikana.

Wafanyikazi waliokuwa wakipanguza uchafu ndani ya kabati hiyo katika kituo cha U-Haul, waliamua kuarifu mamlaka kuu baada ya kifichua unyama huo.

Mabaki ya vijusi hivyo ambavyo vilikuwa karibu vikomae ili vizaliwe vilipatikana vikiwa katika viwango tofauti vya kuoza.

Bi Giesbrecht alikamatwa mara tu baada ya ufichuzi huo.

Wapelelezi bado hawajabaini ikiwa vijusi hivyo viliuliwa baada ya kuzaliwa au vilitolewa vikiwa vimefariki.

Tarehe ya hukumu ya Bi Giesbrecht, haijatolewa.

Post a Comment

 
Top