Seretse Khama na Ruth pamoja na wana wao |
Wakati mwanamfalme wa Kiafrika na karani mmoja mwanamwali Mzungu wa
maisha ya wastani kutoka kwa wamiliki wa bima wa Lloyd, walipoamua
kuoana mnamo mwaka 1948, ilichochea hisia mbalimbali nchini Uingereza na
Afrika.
Seretse Khama alikutana na Ruth Williams alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Oxford na wakaanza kuchumbiana.
Baada ya masomo yake, alitarajiwa kwenda nyumbani hadi katika taifa lake
lililokuwa koloni ya Uingereza wakati huo ikijulikana kama Bechuanaland
ambayo sasa ni Botswana, na kuoa mmoja wa watu wa kabila lake, lakini
mapenzi yake kwa Williams ya libadilisha kila kitu.
Familia yake ilipinga ndoa hiyo na Khama akalazimika kukatalia mbali fursa ya kuwa mfalme.
Serikali ya Uingereza iliingilia kati na kujaribu kupinga ndoa hiyo haua iliyomfanya Khama kufukuzwa kutoka nchi yake.
Askofu wa London, William Wand, angeruhusu tu harusi inayofanyika
kanisani ikiwa tu utawala nchini Uingereza ungeruhusu ndoa hiyo
kufanyika. Hilo halikufanyika.
Wapenzi hao wawili walilazimika kuoana baadaye katika ofisi ya
mwanasheria mkuu iliyoko Kensington huko London mnamo Septemba mwaka
1948.
Waziri mkuu wa Afrika Kusini wakati huo Daniel Malan, alitaja ndoa yao
kama "iliyojaa kichefuchefu" huku mwanafunzi mmoja aitwaye Julius
Nyerere, ambaye baadaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, akasema "ni
mojawepo ya hadithi nzuri sana za mapenzi duniani",
Mmoja wa walioshuhudia alizungumza na dadake Ruth Williams, ambaye alisema harusi hiyo ilikuwa "mapenzi yaliyoshinda chuki".
Wawili hao walipata uungwaji mkubwa huku maandamano yakizidi huko
Bechuanaland, kushinikiza kutambuliwa kwa ndoa hiyo ambapo baadaye
walikubaliwa kurejea nchini humo mnamo mwaka 1956 baada ya watu wa
kabila la Bamangwato, lake Bw Khama, walipoamua kutuma barua kwa njia ya
telegram hadi kwa Malkia Elizabeth wa II.
Kufanikisha uhuru
Seretse Khama aliamua kukatalia mbali utawala wa kabila lake na akaamua
kuwa mkulima na mfugaji huko Serowe. Baadaye alikibuni chama cha
Bechuanaland Democratic Party na akashinda uchaguzi mkuu uliofanyika
mwaka 1965.
Akiwa Waziri mkuu wa Bechuanaland (Botswana) alifanikisha nchi hiyo
kujipatia uhuru mwaka 1966 na akawa Rais wa kwanza wa Botswana.
Ruth Williams Khama, alifahamika kama Lady Khama baada ya uhuru na
alihudumu kama mkewe Rais wa Botswana kuanzia mwaka 1966 hadi 1980.
Walijaliwa watoto wanne: Wa kwanza Jacqueline aliyezaliwa Bechuanaland
mwaka 1950; Ian aliyezaliwa England mwaka 1953, na pacha Anthony na
Tshekedi waliozaliwa Bechuanaland waliozaliwa 1958.
Ian Khama ndiye Rais wa sasa wa Botswana na alianza kuongoza mwaka 2008.
Ian na Tshekedi ni wanasiasa nchini humo.
Post a Comment