Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga,
amewasilisha mpango kazi wake katika kurugenzi ya shirikisho la soka
nchini TFF, ambao utanonyesha namna atakavyofanya kazi katika kipindi
cha miezi sita.
Alfred amesema mpango kazi huo wa Mayanga pia umezingatia michezo ya kufuzu kwa fainali za mataifa bingwa ya Afrika ambapo Tanzania imepangwa kukutana na Rwanda Julai 14 kabla ya kucheza mchezo wa mkondo wa pili Julai 21.
“Mwalimu ameandaa program ambayo atahitaji mechi zote ushindani au hata kama zote zitakuwa ni za kirafiki lakini angalu kipindi cha FIFA week tuwe na mechi mbili aziandae vizuri ili tuweze kufanya vizuri kuonesha ubora wetu wa soka Afrika na ulimwengu kwa ujumla.”
“Ukiachana na michezo hiyo ya Machi 21 mpaka 29, Aprili kati ya tarehe 20 hadi 22 kutakuwa na mechi za kufuzu michuano ya CHAN (mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani) ambapo michuano hiyo itafanyika nchini Kenya.”
“Kati ya Juni 6 hadi 13 kutakuwa na mechi za kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika ambazo zitafanyika mwaka 2009 huko nchini Cameroon.”
Tanzania imepangwa Kundi L katika kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika ambapo wapinzani wake ni Lesotho, Cape Verde na Uganda. JIUNGE NASI KATIKA
Post a Comment