0
Mwanza. Hakimu Mkazi Bahati Chitepo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, amejiondoa kusikiliza kesi inayomkabili Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni jijini hapa, James Chiragwire anayedaiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la tatu.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mkoa, Wilbert Chuma alisema Chitepo amejitoa kusikiliza kesi hiyo kutokana na sababu alizoona zinafaa ili kutenda haki kwa pande zinazohusika.

Alisema Chitepo alifanya hivyo kwa kuzingatia sheria na kwamba, kesi hiyo namba 239/2016 imepangwa kusomwa hoja za awali Februari 8, mbele ya hakimu atakayepangiwa.

Novemba 30, mwaka jana, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Sabina Chogogwe alimsomea mashtaka mshtakiwa mbele ya Hakimu Chitepo akidaiwa kubaka na kumuingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo.

Alidai mshtakiwa ambaye yupo nje kwa dhamana, alitenda kosa hilo Novemba 15, mwaka jana eneo la Nyegezi katika Mtaa wa Nyabulogoya.

Post a Comment

 
Top