0
Kibiti. Watu wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki wameiteketeza nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Jaribu wilayani Kibiti, Ramadhan Msanga baada ya kumkosa nyumbani.

Akisimulia mkasa huo  shuhuda wa tukio hilo, mwalimu Misana Sabatto ambaye ni mpangaji kwenye nyumba hiyo, alisema juzi saa moja usiku akiwa chumbani kwake, alishtuka kuona watu watatu wakiwa na bunduki na wameficha nyuso zao wakiingia na kumtaka awaonyeshe mwenyekiti huyo.

Sabatto alisema watu hao baada ya kubaini wanayemtafuta hakuwapo, walimtaka mwalimu huyo ampigie simu dada yake mwenyekiti huyo, Amina Msanga aende nyumbani hapo.

Akizungumzia tukio hilo, Msanga alisema alipokea simu kutoka kwa mwalimu huyo akimtaka afike nyumbani  hapo kwa kuwa wana matatizo. Alisema alimjibu angefika baada ya dakika 10 kwa kuwa alikuwa akisindikiza wageni.

Hata hivyo, alisema akiwa anasindikiza wageni alipokea simu kutoka kwa dada yake mwingine ikimjulisha kuwa wapo nyumbani kwa kaka yao na nyumba imechomwa moto.


Post a Comment

 
Top