Kesi iliyowasilishwa kwenye mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe na
kiongozi wa maandamano Promise Mkwananzi, ya kupinga utawala wa Rais
Robert Mugabe imetupilikwa mbali.
Kundi la Tajamuka lilitaka kuonyesha kuwa raia Mugabe mwenye umri wa
miaka 92 hayuko katika hali nzuri kuongoza kutokana na umri wake.
Mahakama ilitulipia mbali kesi hiyo ikisema kuwa bwana Mkwananzi alishindwa kumkabidhi Mugabe makaratasi ya kesi.
Sasa Mkwananzi ana siku 30 za kuchukua hatua zinazohitajika kabla ya kupeleka tena kesi hiyo mahakamani.
Promise Mkwananzi |
Post a Comment