Afisa tarafa ya Mhukuru Salma Mapunda amesema kuwa kabla ya tukio hilo la kinyama watu hao waliwahi kuzingirwa nyumbani kwao hali iliyomlazimu mtendaji wa kijiji cha Nakahegwa kukodi pikipiki na kuwapakiza wote wawili usiku wakiongozwa na mgambo wa kijiji kuwapeleka kituo kidogo cha polisi kata ya Magagula kabla ya kufika kundi la watu wakiwa na mapanga waliwavamia na kuanza kuwapiga ambapo Mzee severin Mgogo alipoteza maisha na Antony hali yake ni mbay yupo hospitali ya misheni Peramiho.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Mgema ametembelea kijijini hapo na kufanya mkutano wa hadhara amemwagiza mkuu wa kituo cha polisi kuwakamata viongozi wa kijiji mwenyekiti na kamati yake hatimaye hatua za kisheria zichukuliwe kwa kosa la kushindwa kutatua tatizo hilo kwa wakati.
Mtoto wa marehemu John Mgogo ameiomba serikali kuchukua za haraka za kuwasaka waliofanya tukio hilo.
Post a Comment