Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imeridhia ombi lililowasilishwa
Mahakamani hapo na upande wa Jamuhuri la kuwakata watuhumiwa 8 wa Dawa
za kulevya kuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka 3,huku
wakitakiwa kufika katika Kanda maalum ya Dar es Salaam Mara mbili kwa
mwezi.

Ambapo
kwa mujibu wa Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo akisoma maamuzi ya
Mahakama Huruma Shaibu amesema Mahakama imeridhia ombi hilo ambapo
watuhumiwa hao watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja
tofauti na ombi la Jamuhuri la miaka mitatu, lakini pia ameagiza Jeshi
la Polisi kuwafanyia uchunguzi wa Mara kwa Mara katika maeneo yao, na si
kufika kituo cha Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam kama Jamuhuri
ilivyoomba.
Post a Comment