VIPODOZI aina mbalimbali vyenye ujazo wa tani kumi, vimenaswa na
kuzuiliwa katika kituo cha ukaguzi mizani ya Makambako mkoani Njombe
vikielekea Jijini Dar es salaa.
Shehena hiyo imekutwa ikiwa katika magari mawili yote ya kampuni ya
Kisima Company Limited. Ya jijini Dare s salaam iliyokuwa ikitokea
nchini Kongo, katika tukio hilo watu watatu wanashikiliwa kati sita
waliokuwemo ndani ya magari hayo wakiwemo madereva wawili na wasaidizi
wao.
Magari hayo ni aina ya FAW yakusafirishia mafuta, yamekamatwa usiku wa
februari 5 saa 5 za usiku yakitokea nchini Zambia kuelekea jijini Dar es
salaamu.
Tukio hilo limehusisha gari aina ya FAW lenye namba T. 807 CHK na trela
lenye namba T. 750 DDE na gari jingine namba T. 813 CHK yalikamatwa
February 5 mwaka huu katika mizani ya Makambako.
Mhandisi Ruth Shallua ni msimamizi mkuu wa kituo cha mizani ametoa
maelezo ya tukio hilo mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe, Cgrstopher Ole
Sendeka na kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe, Prodensia Protus ambao
walifika kushuhudia tukio hilo katika kitupo cha polisi wilaya ya
kipolisi Makambako.
Upande wake mkuu wa mkoa anasisitiza kupatikana kwa wathumiwa watatu waliotoroka mkono wa sheria.
Amesisitiza kujipanga kupambana na matukio kama hayo ikizingatia kuwa
barabara hii huenda kuna magendo zaidi ya hayo yanafanyika pasipo
kujulikana.
Uchunguzi zaidi wa mamlaka ya chakula na dawa umefika na kuendelea na
ukaguzi wa mzigo huo, ili kutoa thathimini na thamani ya shehena hiyo.
Post a Comment