Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimelaani kitendo cha Jeshi la
Polisi kumkamata Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho na Mbunge wa Singida
Mashariki Tundu Lisu kwa kile ilichodai bila kuzingatia kanuni na
taratibu za Bunge huku ikilitaka Jeshi hilo kumwachia Mbunge huyo kwa
dhamana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaaam Katibu Mkuu wa
CHADEMA Dk. Vicent Mashinji amedai kitendo kilichofanywa na Jeshi hilo
cha kumkamata Tundu Lisu akiwa katika maeneo ya Bunge ni uvunjifu wa
haki na Kinga za Wabunge ambapo amedai kuwa Jeshi hilo linatumika
kuingilia siasa za Upinzani.
Wakati huhuo Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimezungumzia
kuhusu Tuhuma zinazomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe
kuhusiiana na kutajwa kwenye Orodha ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na
dawa za kulevya.
Post a Comment