Mkoa wa Simiyu umetajwa kushika nafasi ya 64 katika uzalishaji wa zao la
Pamba duniani ,ambapo hapa nchini unaongoza kwa kuzalisha kwa asilimia
50 ili kuweza kuwa Miongoni Mwa Mataifa 10 Bora ,Kilimo Kinapaswa
kifumuliwe kiwe cha Kisasa pia Wakulima wahamasishwe kutilia mkazo
kwenye pamba ya organiki ili kuongeza Mnyoyoro wa thamani wa zao hilo
hasa katika Soko la dunia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kuwasilisha Mwongozo wa
uwekezaji Mkoani Simiyu katika kikao kilichowashirikisha wawekezaji
wazawa ,wajumbe wa kamati za fedha na Uchumi wa Halmashauri sita ,Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji lengo kuu ni uhamasishaji na
kuendeleza uwekezaji ,Mtafiti Mwandamizi Taasisi ya Utafiti na Mambo ya
Uchumi (ESRF) Bamwenda Gration ,
Amesema kuwa Simiyu ina fursa nyingi katika kilimo cha Mazao yenye
thamani kubwa na yanayoweza kusindikwa ,kuchakatwa ,bidhaa zitokanazo na
mifugo na maendeleo endelevu ya viwanda kuanzia viwanda vya bidhaa
zitokanazo na Pamba Alizeti ,na Mazao ya Mikunde na ili kuongeza Pato la
Mwananchi Simiyu ifikapo 2050 kutoka dola 3,600 hadi 12,000 lazima
kilimo kiwe na tija .
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema mkoa unatekeleza miradi
ambayo inalenga hasa katika sekta ya viwanda na tayari wilaya za maswa
na meatu zimetoa nafasi ya umiliki wa mitazamo na umiliki wa dira kama
mkoa na umiliki wa mawazo kwenda ngazi ya chini zaidi.
Post a Comment