Kiteto.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Kiteto,
Tumaini Magesa na mkurugenzi wa halmsahuri ya wilaya hiyo, Tamim
Kambona waende Kata ya Engusero Jumamosi wiki hii wakafanye mkutano wa
hadhara na kujibu kero za wananchi wa kata hiyo.
Wametakiwa pia wafuatane na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Lairumbe Mollel wakatoe ufafanuzi bila kukosa.
Majaliwa ametoa agizo hilo leo katika kijiji cha Engusero wilayani
kiteto baada ya kusimamishwa na wananchi wakati akiwa njiani kuelekea
mjini Kibaya yalipo makao makuu ya wilaya hiyo ili aanze ziara ya kikazi
ya Mkoa wa Manyara.
Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha
Engusero, Waziri Mkuu amesema analichukua ombi la wakazi hao la kupata
kujengewa
Post a Comment