Chama cha Akiba na mikopo cha wananchi wa kijiji cha Uswaa Mamba wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambao wanajishughulisha na kilimo na biashara ndogondogo kiko hatarini kufaa baada ya viongozi wa bodi kutuhumiwa kukopeshana akiba za wanancachama zaidi ya shilingi milioni 100 kinyume cha sheria.
Wanachama hao wamesema wanasikitishwa na hatua ya viongozi hao
kusababisha ubathirifu huo ambao kwa sasa umesababisha wananchama hao
kukosa mikopo ya kuwawezesha kufanya shughuli za maendeleo kama
ilivyokusudiwa
Wamesema kwa vema viongozi hao wakataifishwa mali zao kwa kuwa chama
hicho kwa sasa kina mtaji wa shilingi milioni 25 ambazo hazitoshelezi
kutokana na wengi wao kushindwa kupata mikopo kwa ajili ya kulipia
watoto wao ada,kilimo
Afisa ushirika wilaya ya hai bw. Paul ndulu amesema viongozi hao
watawajibishwa kutokana na wao kuhusika kusababisha hasara hiyo
ambayo imesababisha wananchama zaidi ya 1500 kukosa mikopo.
Meneja wa chama hicho bw. Shirilengwa ulomi amethibitisha kuwepo kwa
ubathirifu huo tangu mwaka 2013 ambapo viongozi walijiidhinishia fedha
hizo kinyume cha sheria hali ambayo imesababisha chama hicho kuanza
kuzorota.
Post a Comment