Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
Kanuni hizo zimeeleza kuwa mmiliki wa nje akitaka kuomba leseni kwa Mkurugenzi wa Idara za Huduma ya Habari atatakiwa kuorodhesha wamiliki wenza wa ndani ambao atashirikiana nao watakaokuwa na hisa zisizopungua asilimia 51.
Pia, mmiliki mmoja au kikundi cha watu ambao ni wazawa kanuni hazijaweka mipaka ya hisa wanazotakiwa kuwa nazo katika umiliki wa kampuni ya gazeti. Kanuni hizo zinaunga mkono Sera ya Habari ya mwaka 2013 na Sheria ya Huduma ya Utangazaji ya mwaka 1993 ambayo inamtaka mmiliki wa chombo cha habari kutoka nje asizidi asilimia 49 za umiliki wake.
Post a Comment