Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Zanzibar ambao pia ni wawakilishi
wa Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika timu
ya Zimamoto itaondoka Visiwani Zanzibar leo saa 9:00 alasiri katika
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakilekea mjini
Beira, Msumbiji kucheza mchezo wa mkondo wa pili na wenyeji wao timu ya
Ferroviario de Beira pambano litakalopigwa Jumamosi hii ya Februari 18,
2017 huko Beira.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Jumamosi iliyopita Amani
Mjini Unguja wenyeji Zimamoto waliifungaFerroviario de Beira kwa mabao
2-1 ambapo katika mchezo wa marejeano Zimamoto wanalazimika kupata japo
sare ili kusonga mbele katika hatua nyingine ya kombe hilo kubwa kwa
vilabu barani Afrika.
Post a Comment