0
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Zanzibar ambao pia ni wawakilishi wa Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Zimamoto  itaondoka Visiwani Zanzibar leo saa 9:00 alasiri katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakilekea mjini Beira, Msumbiji kucheza mchezo wa mkondo wa pili na wenyeji wao timu ya Ferroviario de Beira pambano litakalopigwa Jumamosi hii ya Februari 18, 2017 huko Beira.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Jumamosi iliyopita Amani Mjini Unguja wenyeji Zimamoto waliifungaFerroviario de Beira kwa mabao 2-1 ambapo katika mchezo wa marejeano Zimamoto wanalazimika kupata japo sare ili kusonga mbele katika hatua nyingine ya kombe hilo kubwa kwa vilabu barani Afrika.

Post a Comment

 
Top