Hatimaye Klabu ya Simba SC imelipa kodi iliyokuwa inadaiwa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya nyasi bandia walizokuwa
wamezitelekeza bandarini mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya TRA kutangaza kuzipiga mnada nyasi hizo
endapo wangeshindwa kukomboa kwa siku 14 waliozokuwa wamepewa ambazo
zilimalizika juzi Jumanne.
"Mpaka sasa tumeshalipia kodi yote ya nyasi bandia, kinachoendelea sasa
hivi ni wakala wetu kumalizia taratibu za kutoa 'container' zenye nyasi
hizo bandarini kwenda kuwekwa rasmi katika uwanja wetu wa Bunju".
Alisema Makamu wa Rais wa klabu ya hiyo Geofrey Nyange 'Kaburu'.
Kwa upande mwingine klabu hiyo inaendelea kujiandaa na mchezo ujao wa
ligi kuu dhidi ya Mbao FC unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa CCM
Kirumba Jijini Mwanza Jumatatu ijayo.
Post a Comment