Msanii wa muziki wa kizazi kipya TID Mnyama amefunguka na kusema sasa
hivi watu ambao mwanzo walikuwa wakimpa support kwenye muziki na mambo
yake mengine wamemtosa na hawampi msaada wowote hivyo kila kitu
anapambana mwenyewe.
TID amesema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na
kusema watu hao wameacha kumpa suport baada ya yeye kuachana na madawa
ya kulevya hivyo saizi wao wanamuona yeye ni kama msaliti.
"Saizi kila kitu nafanya mwenyewe hata hao mabrother unaosema
washanitosa maana wao walikuwa wanapenda kuona nazidi kuharibika, hivyo
toka nimetangaza kuachana na madawa ya kulevya wao wananiona mimi kama
'snitch', lakini hilo halina tatizo kwani mimi mwenyewe niko vizuri
ndiyo maana unaweza kuona video hii nimetumia pesa nyingi kuifanya na
nimelipa mwenyewe, hii pesa ningesema ninue gari basi ningepata Mark X
nyingine lakini nimeamua kuiweka kwenye video ili kuleta ubora zaidi"
alisema TID
TID leo ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Woman' na kusema siku yoyote ataachia video ya ngoma.
Post a Comment