Mwanamuziki Kriticos wa nchini Ubelgiji leo amewasili nchini kwa lengo
la kufanya wimbo pamoja na msanii chipukizi wa Tanzania anayekuja kwa
kasi sana, ajulikanae kama Harmorapa.
Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere mchana leo, mwanamuziki Kriticos ambaye anaimba miondoko ya
kufokafoka ‘rap’, amesema kuwa anavutiwa na aina ya uimbaji ya Harmorapa
na ndiyo sababu kuu iliyomfanya aje hapa nchini ili kufanya naye kazi.
Kwa upande wake Harmorapa anayetamba na kibao chake cha Kiboko ya
Mabishoo alichomshirikisha Juma nature, amesema kuwa ujio huo kwake ni
heshima kubwa na utamfanya atambulike zaidi kimataifa.
Pia amewataka mashabiki wake kukaa mlo wa kula. Ngoma hiyo itatengenezwa na kurekodiwa na mtayarishaji wa muziki, P-Funk majani.
Post a Comment