Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" ametangaza vita dhidi ya kundi la wanamgambo la al-Shabab.
Ametoa pia msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo hao, akiwataka kujisalimisha, ili wapate mafunzo, ajira na elimu.
Hi ni baada ya shambulizi la kujitoa mhanga kutokea karibu na jengo moja
la serikali mjini Mogadishu ambapo watu 7 waliuawa pamoja na misururu
ya kutekwa nyara kwa wafanyakazi wa kutoa misaada katika taifa hilo
linalokumbwa na ukame.
Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlaka
Mashambulizi yamekuwa ya mara kwa mara na vikosi vyote nchini Somalia
vimekuwa katika hali ya tahadhari ili kukabiliana na tisho lolote kwa
usalama.
Pia amesema kuwa amewafanyia mabadiliko maafisa wa vyeo vya juu kwenye
idara ya ujasusi na polisi ili kujiandaa katika vita dhidi ya al-Shabab.
Post a Comment