Hekaheka ya leo April 6 2017 kupitia Leo Tena ya Clouds FM imetokea
katika kata ya Imesela mkoani Shinyanga ambako kulikuwa na tatizo la
wanafunzi kukumbwa na mapepo wakati wa masomo, lakini sasa unaambiwa
mbali na tukio hilo ambalo lili-make headlines kuna tukio lingine.
Katika kijiji hicho kunadaiwa kuwepo Mti ambao ukiukaribia unapiga shoti
ukidaiwa kuwa na mapepo ambayo wanafunzi wamekuwa wakiongea nayo
kupitia mti huo wanapokumbwa na mapepo huku pia kijiji hicho kikiwa na
Fisi wengi wanaochukuliwa kama paka na wanakijiji.
Post a Comment