0

 Mchezo wa mpira wa miguu unatajwa kuwa na mashabiki wengi duniani na huvutia watu wa jinsia na rika zote. Leo millardayo.com inakusogezea list ya  maajabu kumi yaliyotokea katika mchezo wa  SOKA duniani.

1.Mwanasoka mkongwe wa Brazil Pele, alijipatia jina hilo la utani lenye maana katika lugha ya kibrazil na kireno “ miguu sita” (six feet), kutokana na kuwa na vidole sita katika kila mguu. Jina la halisi ni Edson Arantes do Nascimento
 2.Mwanasoka anakimbia kilomita zipatazo kumi (10) katika mchezo mmoja.
 3.Mwanasoka toka nchini Brazil, Ronaldinho ndio mfungaji anayekumbukwa zaidi kwa kufunga mabao mengi duniani, alifunga mabao 23 akiwa na umri wa miaka 13 tu.
 4.Mnamo mwaka 1998 radi iliua wachezaji wote kumi na moja (11) wa timu moja na kuacha wachezaji wa timu pinzani wakati wa mchezo nchini DRC na kuathiri watazamaji wapatao thelathini.
 5.Mnamo mwaka 1964 simu aliyopokea mwamuzi wa mchezo (refa) akiwa uwanjani huko nchini Peru ilisababisha vurugu iliyopelekea watu mia tatu (300) kufariki.
 6.Mashabiki wa soka nchini Columbia waliingia na jeneza uwanjani la mshabiki mwenzao aliyeuawa kwa kupigwa risasi siku ya mchezo kuwania kuingia fainali akiwa na umri wa miaka17. Mashabiki hao waliingia nae siku ya fainali.
 7.Mnamo mwaka 1966 Kombe la Dunia liliibiwa na baadae mbwa akalipata siku chache kabla ya mshindano hayo kuanza. Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza lilitengenezwa kwa makaratasi na kubadilishwa baada ya kuharibiwa na mvua kubwa iliyonyesha. Siku hizi Kombe hilo linatengenezwa na dhahabu yenye uzito upatao kilo 4.97.
 8.Katika Kombe la Dunia mwaka 1950, timu ya Soka ya India ilitaka kucheza peku, Shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) likagoma. Timu hiyo ikasusia mashindano hayo.
 9.Pele alipoenda Nigeria kucheza soka katika mchezo wa hisani mnamo mwaka 1967, pande mbili zilizokuwa zikipigana vita, zilikubaliana kusimamisha vita kwa muda wa masaa 48.
 10.Martinho Eduardo Orige kutoka Brazil ndie anatufungia list hii huyu ni mchezaji pekee mwenye uwezo wa kuchezea mpira kwa muda mrefu zaidi duniani! Alichezea mpira kwa muda wa saa 19.5, alivunja record hiyo mnamo mwaka 2003.

Post a Comment

 
Top