WAKONGWE wa soka nchini Italia, AC Milan wamefungiwa kushiriki michuano ya Ulaya kwa mwaka mmoja kutokana na kukiuka kanuni za soka.
Timu hiyo ilikuwa ikijiandaa kushiriki katika michuano ya Europa League msimu ujao wa 2018/19 baada ya kushika nafasi sita katika Serie A msimu uliopita.
Chanzo cha kufungiwa ni kukiuka kanuni ya masuala ya fedha (Financial Fair Play) ambapo imeelezwa kuwa klabu hiyo imekuwa ikipoteza mapato mengi kila mwaka kwa kutokuwa na hesabu nzuri za kifedha.
Milan inayonolewa na Gennaro Gattuso ipo hatarini kupoteza mastaa wake wengi licha ya kuwa chini ya umiliki wa bilionea wa China, Li Yonghong. Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) limetoa nafasi ya Milan kukata rufaa.
Post a Comment