0

WAZIRI wa viwanda, biashara na uwekezaji, Charles Mwijage amewataka wafanyabiashara nchini kuzalisha kwa viwango na tija kulingana na viwango vya kimataifa.

Akizungumza  mara baada ya kufanya ziara ya kukagua mabanda ya Maonyesho  42 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) yanayofanyika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji wa Biashara Tanzania (Tantrade) ambapo watakutana wajasiliamali na wazalishaji wakubwa kutoka ndani na nje ya nchi, Mwijage amesema kama wafanyabiashara wa Tanzania watashindwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali katika kuboresha biashara zao ni wazi kwamba nchi itakua imepoteza fursa adhimu kibiashara.

Amesema mbali na maonyesho hayo serikali itatoa matrekta elfu 2400 kwa wakulima wakubwa na wakati ambayo yatakwenda shambani kwaajili ya kukuza kilimo cha kisasa na kuzalisha kwa tija ili viwanda vipate malighafi za kutengeneza bidhaa kwa

Maonyesho ya 47 ya Sabasaba yanatarajiwa kufunguliwa na waziri Mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli Jumatatu ya Jualai 2, 2018.Zaidi ya  makampuni 500 na nchi zaidi ya 20 zimejiandikisha kushiriki maonyesho hayo.

Post a Comment

 
Top