0

Kocha wa zamani wa Simba, Dylan Kerr ametoa onyo kwa waajiri wake hao wa zamani akiweka  msisitizo kuhusiana na suala la kiungo Francis Kahata.

Kerr ambaye sasa ni kocha wa mabingwa wa Kenya, Gor Mahia amesema Kahata bado ana mkataba na klabu yake na Simba wanapaswa kuheshimu hilo.

"Lazima waonyeshe nidhamu ya mkataba, Kahata ana mkataba na Gor Mahia, wasifanye mambo kienyeji.

"Kuna mambo yamekuwa yakiendelea. Hili si jambo sahihi na lazima vitu vifuate weledi," alisema.

Kumekuwa na taarifa kwamba Simba inaendelea kumnyatia Kahata ambaye ni kiungo mchezeshaji tegemeo wa klabu hiyo kongwe na maarufu zaidi nchini Kenya.

Tayari Simba imefanikiwa kumsajili Meddy Kagere ambaye ni mshambulizi tegemeo wa Gor Mahia, jambo ambalo limeonyesha kumkera kocha huyo raia wa Uingereza.

Kerr amekerwa na hatua hiyo ya Simba kwa kuwa Kagere aliaga anarejea kwao Rwanda kushughulikia suala la pasi ya kusafiria, lakini akatua Dar es Salaam na kumalizana na Simba.

Post a Comment

 
Top