Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi Ajira na
Vijana) Bibi Jenista Mhagama amesema serikali itakaa na wadau ili
kuangalia namna ya kulimaliza sakata la fao la kujitoa katika mifuko ya
hifadhi ya jamii.
Waziri
Mhagama ametoa kauli hiyo jana katika mkutano wa sita wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) mjini Dodoma uliofunguliwa leo na Waziri
Mkuu Mjini Dodoma, ambapo katika risala yake, TUCTA ilihoji kuhusu
marekebisho ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na ucheleweshwaji wa malipo ya
pensheni.
Mhagama alisema
kuwa baada ya uongozi wa TUCTA kukamilika, itabidi wakutane na kukaa
pamoja kuainisha sera inataka nini na hali ya uchumi ya sasa ikoje huku
wakiangalia dhana nzima ya hifadhi ya jamii nayo inataka nini.
“Kuna
haja ya kuangalia sera inataka nini, tunapaswa tuangalie mabadiliko ya
kiuchumi katika nchi yetu na kutazama dhana nzima ya hifadhi ya jamii
kwenye maisha yetu ya uzeeni. Tukikaa pamoja, yaani, mwajiri, mfanyakazi
na Serikali, tutapata njia ya kisheria ya kuweza kulifunga jambo hili
ili lisiendelee kuwa kero kwa wafanyakazi wetu,” alisema.
Post a Comment