Waislamu wote nchini wametakiwa kuadhimisha Siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu.
Aidha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Siku ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Hata hivyo, ugeni rasmi wa Waziri Mkuu Majaliwa unategemea ratiba yake.
Hayo
yalisemwa jana Dar es Salaam na Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar
Zubeir wakati akizungumzia Siku ya Maulid ambayo alisema kwa mwaka huu,
Maulid itasomwa usiku wa Desemba 11, na kitaifa itafanyika Kata ya
Shelui wilayani Iramba Mkoa wa Singida na mapumziko yatakuwa siku
inayofuata yaani Desemba 12.
Mufti
Zubeir alisema Waislamu wanatakiwa kutumia siku hiyo kuonesha matendo
mema na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu pamoja na kuisaidia jamii
kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuchangia damu ili kusaidia wenye
uhitaji huo.
Alisema
anatakiwa kiongozi kufanya matendo hayo wanapoifurahia siku ya kuzaliwa
Mtume Muhammad (S.A.W) ambaye amesema uislamu ni usafi, basi
jisafisheni wenyewe.
“Mimi
na familia yangu tutafurahia siku hiyo kwa kufanya usafi mtaani kwetu
Mikocheni na kuchangia utoaji damu ili kusaidia watu wenye uhitaji,” alieleza
Mufti Zubeir na kuwataka Waislamu kutokujiingiza kwenye makundi ya
ugaidi kwani Uislamu sio ugaidi na kuwasihi waachane na hizo tabia.
Post a Comment