Mashirika kadhaa makubwa ya habari yameelezea masikitiko yao kuhusu
kitendo cha kuzuiwa kuhudhuria mkutano wa wanahabari uliofanyika Ikulu
ya White House, Marekani.
Wasimamizi wa Gazeti la The New York Times na shirika la utangazaji CNN wamesema hali hiyo haikubaliki kamwe na kuitaja kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya nchi hiyo.
Mkurugenzi wa shirika la habari la the New York Times Dean Baquet amesema jambo kama hilo halijawahi kutokea katika historia ya nchi na hata gazeti hilo.
Amesema uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa kuweka uwazi kwenye shughuli za kiserikali kwa niaba ya maslahi ya umma.
Msemaji wa rais wa Marekani Donald Trump , Sean Spicer awali alikuwa amedai kuchukua hatua hiyo kwa sababu hawawezi kukaa kando na kuachia uenezwaji wa habari za uongo.
Rais Trump amekuwa akiviita maadui wa raia wa Marekani vyombo kadhaa vya habari nchini humo ikiwemo na The New York Times.
Mkutano huo ambao kwa kawaida hutoa taarifa za serikali kila siku na kurushwa moja kwa moja, kupitia televisheni, dakika za mwisho iliamuriwa usionyeshwe na ni wanahabari wachache waliruhusiwa kuhudhuria.
Baadhi ya vyombo vya habari, vilivyozuiwa kuingia kwenye mkutano huo vinatuhumiwa kutoa habari zinazokosoa serikali ya Rais Donald Trump.

Post a Comment