Kuhusu ndugu wa marehemu, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, George
Salala alisema ndugu zake bado hawajajitokeza na wanaendelea
kuwasiliana na madaktari kujua chanzo cha kifo na Jackline. Alisema hadi
juzi zaidi ya Watanzania 2,000 walikuwa wamerudi nchini.
Jackline Grayson, ambaye amefariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara Ligula baada ya kurudishwa nchini kutoka Msumbuji, anadaiwa kuwa
na wadogo zake wawili wanaoishi Ubungo Maziwa, Dar es Salaam na kwamba
ni mwenyeji wa Njombe.
“Msumbiji alikuwa anafahamika kwa jina la Jackline Grayson, lakini
nimesikia jina la nyumbani kwao ni Josephine Sanga. Dar es Salaam ana
wadogo zake wawili ni vyema kama wakisikia taarifa hizi (wajitokeze),”
alisema Agnes John ambaye anatunza mtoto wa marehemu.
Akiwa anajipanga kuanza upya maisha, Agnes, mmoja wa Watanzania
waliotimuliwa Msumbiji, anakabiliwa na mambo mawili mazito; kumpoteza
rafiki yake na kusaka ndugu wa mtoto wa mwaka mmoja aliyeachiwa.
Agnes, ambaye ni mwenyeji wa Mbeya, anaishi na Watanzania wengine
waliorejeshwa nchini katika mahema yaliyowekwa Uwanja wa Mashujaa mjini
hapa kusubiri kupiga hatua nyingine baada ya harakati zao za kutafuta
maisha Msumbiji kukatishwa ghafla.
“Siwafahamu ndugu wa marehemu,” alisema Agnes na kuongeza: “Naomba ndugu
zake wajitokeze ili kumzika na kufanya uamuzi kuhusu mtoto wake
Post a Comment