0
Mlinzi wa kati wa Simba, Abdi Banda ameomba radhi kwa mashabiki wa soka nchini kwa kitendo chake cha kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Banda alikuwa mwenye bahati kwa kutotolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumtwanga ngumi Kavilla Jumapili katika mchezo ambao Simba ililala 2-1 kutokana na tukio hilo kutoonwa na waamuzi.

Katika kauli yake, Banda hajaeleza kwa uwazi kitu gani hasa alichokifanya na sababu za kufanya kitendo kile ambacho kilionekana dhahiri katika picha za video.

“Nachukua nafasi hii kuwaomba radhi watanzania na kaka yangu (Kavilla) kwa tukio lilitokea Jumapili, kwa sababu mimi na yeye ndiyo tunajua kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea,” amesema Banda.

Post a Comment

 
Top