0
Zaidi ya wajasiriamali 20 wanatarajia kwenda nchini china kushiriki maonyesho ya kibiashara ya Guangzhou, yaliyopangwa kuanza Aprili 14 hadi 20 mwaka huu, yakishirikisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Safari ya wafanyabiashara hao wa kitanzania inaratibiwa na Taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF kwa kushirikiana na Kampuni binafsi ya Kinyago Travel na Tours ya Dar es Salaam, ambazo kwa pamoja zimelenga kuhakikisha ushiriki wa Tanzania kwenye maonyesho hayo unakuwa wa mafanikio.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kinaygo Diana Gaspar na baadhi ya wajasiriamali watakaoshiriki maonyesho hayo, wanaeleza ni kwa namna gani Tanzania itanufaika na maonyesho hayo.

Post a Comment

 
Top