MANCHESTER, England
WAKATI dirisha dogo la usajili la Januari likinukia, tayari kuna orodha ndefu ya mastaa wanaotakiwa na makocha wa Ligi Kuu England.
Wengi wao wameshatajwa kwenye mipango ya baadaye ya klabu zao au katika klabu nyingine.
Ukiiangalia Manchester United, bado haijarudi kwenye ubora wake wa miaka kadhaa iliyopita.
Ni ngumu kukifananisha kikosi cha sasa cha Old Trafford na kile cha miaka 10 iliyopita.
Mbali na Sir Alex Ferguson, makocha wote waliomfuata wameshindwa kuirudisha Man United katika zama zake.
Hata hivyo, ni wachezaji gani ambao Jose Mourinho anatakiwa kuachana nao pindi dirisha dogo la usajili
litakapofunguliwa Januari?
Akiwa chini ya kocha Louis van Gaal, ambaye ndiye aliyemsajili, Depay alicheza mechi 45 katika msimu wa mwisho wa Mholanzi huyo.
Si tegemeo kwenye kukosi cha sasa cha Mourinho, ingawa kocha huyo amekuwa akikiri kuwa anaumia kumweka benchi Depay.
Depay ametokea benchi mara saba kwenye kikosi cha Mourinho na kuanza mara moja. Mpaka sasa, nyota huyo amecheza dakika 134 pekee.
Roma na Everton wameonyesha nia ya kumsajili staa huyo na huenda ikawa vema kwa Man United kumfungulia mlango wa kutokea.
Msimu uliopita, ni wachezaji sita pekee ambao walicheza mechi nyingi kuliko Schneiderlin.
Tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi, mkali huyo amecheza dakika 11 tu kwenye kikosi cha Mourinho.
Mtandao wa Daily Telegraph umenyetisha kuwa, kiungo huyo anawaniwa na Everton.
Hata hivyo, Schweinsteiger amerejea kwenye kikosi cha kwanza cha Man United, na mwezi uliopita alicheza mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya West Ham.
Hiyo imeibua shaka kuwa huenda bado Mourinho anahitaji uwepo wa nyota huyo Old Trafford.
Lakini, bado Schweinsteiger hajajihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza, hivyo kuna uhakika mkubwa kuwa atatafuta njia ya kutokea Old Trafford.
Kumekuwa na taarifa kuwa, staa huyo anawindwa na baadhi ya klabu za Ligi Kuu nchini Marekani (MLS).
Mmoja wa mabosi wa MLS, Don Garber, aliwahi kusema kiungo huyo mwenye umri mwa miaka 32 anakaribishwa nchini Marekani.
Kwa sasa hali yake ni mbaya tangu kutua kwa Mourinho, kwani amekuwa akiingia uwanjani mara chache.
Itakumbukwa kuwa, Young ameozea benchi tangu Novemba alipocheza mchezo wa ligi dhidi ya Swansea, ambapo kikosi chake kiliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Mechi ya mwisho kuingia kwenye kikosi cha kwanza ilikuwa ni ile ambayo Man United ilitoa sare na Liverpool.
Alipoulizwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports kwanini Young hapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake, Mourinho alikejeli, akidai nyota huyo amezoea mechi kubwa.
Tangu alipotoa kaluli hiyo, Young ameingia uwanjani mara mbili pekee.
Hakuna uhakika wa Mwingereza huyo kubaki Old Trafford, hasa baada ya klabu kadhaa kuvutiwa na saini yake.
Moja kati ya timu za Ligi Kuu England ambazo zimeonyesha nia ya kumhitaji staa huyo ni mabosi wake wa zamani, Watford.
WAKATI dirisha dogo la usajili la Januari likinukia, tayari kuna orodha ndefu ya mastaa wanaotakiwa na makocha wa Ligi Kuu England.
Wengi wao wameshatajwa kwenye mipango ya baadaye ya klabu zao au katika klabu nyingine.
Ukiiangalia Manchester United, bado haijarudi kwenye ubora wake wa miaka kadhaa iliyopita.
Ni ngumu kukifananisha kikosi cha sasa cha Old Trafford na kile cha miaka 10 iliyopita.
Mbali na Sir Alex Ferguson, makocha wote waliomfuata wameshindwa kuirudisha Man United katika zama zake.
Hata hivyo, ni wachezaji gani ambao Jose Mourinho anatakiwa kuachana nao pindi dirisha dogo la usajili
litakapofunguliwa Januari?
Memphis Depay
Alisajiliwa kutoka PSV Eindhoven na uhamisho wake uligharimu pauni milioni 31.Akiwa chini ya kocha Louis van Gaal, ambaye ndiye aliyemsajili, Depay alicheza mechi 45 katika msimu wa mwisho wa Mholanzi huyo.
Si tegemeo kwenye kukosi cha sasa cha Mourinho, ingawa kocha huyo amekuwa akikiri kuwa anaumia kumweka benchi Depay.
Depay ametokea benchi mara saba kwenye kikosi cha Mourinho na kuanza mara moja. Mpaka sasa, nyota huyo amecheza dakika 134 pekee.
Roma na Everton wameonyesha nia ya kumsajili staa huyo na huenda ikawa vema kwa Man United kumfungulia mlango wa kutokea.
Morgan Schneiderlin
Ni mchezaji mwingine ambaye alisajiliwa na Van Gaal mwaka 2015. Amechemsha tangu Mourinho alipotua Old Trafford.Msimu uliopita, ni wachezaji sita pekee ambao walicheza mechi nyingi kuliko Schneiderlin.
Tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi, mkali huyo amecheza dakika 11 tu kwenye kikosi cha Mourinho.
Mtandao wa Daily Telegraph umenyetisha kuwa, kiungo huyo anawaniwa na Everton.
Bastian Schweinsteiger
Mourinho aliposema kuwa haitakuwa rahisi kwa Schweinsteiger kucheza kwenye kikosi chake, ilionekana wazi kuwa Mjerumani huyo angeondoka Januari.Hata hivyo, Schweinsteiger amerejea kwenye kikosi cha kwanza cha Man United, na mwezi uliopita alicheza mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya West Ham.
Hiyo imeibua shaka kuwa huenda bado Mourinho anahitaji uwepo wa nyota huyo Old Trafford.
Lakini, bado Schweinsteiger hajajihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza, hivyo kuna uhakika mkubwa kuwa atatafuta njia ya kutokea Old Trafford.
Kumekuwa na taarifa kuwa, staa huyo anawindwa na baadhi ya klabu za Ligi Kuu nchini Marekani (MLS).
Mmoja wa mabosi wa MLS, Don Garber, aliwahi kusema kiungo huyo mwenye umri mwa miaka 32 anakaribishwa nchini Marekani.
Ashley Young
Maisha ya Young pale Old Trafford yalikuwa matamu wakati wa utawala wa Van Gaal.Kwa sasa hali yake ni mbaya tangu kutua kwa Mourinho, kwani amekuwa akiingia uwanjani mara chache.

Post a Comment