Baada ya Serikali kuufungulia Uwanja wa Taifa, TFF yatoa tamko kuhusui Simba na Yanga
Muda mfupi baada ya serikali kupitia Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Nape Nnauye kutangaza kuufungulia Uwanja wa Taifa kwa ajili
ya matumizi ya michezo na shughuli nyingine za kijamii, Shirikisho la
Soka la Tanzania (TFF) limetoa tamko.
TFF imetangaza kuwa kutokana na ruhusha hiyo, sasa michezo ya wikiendi
hii inayozihusisha Simba na Yanga ni rasmi itafanyika kwenye uwanja huo
ambao ni mkubwa kuliko vianwaj vyote vya michezo nchini.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema:
“Nachukua nafasi hii kumshuru rais wetu Magufuli na serikali kwa jumla
kwa kuweza kuamua kuufungua Uwanja wa Taifa uanze kutumika na timu za
Simba na Yanga ambazo zilifungiwa kuutumia.
“Nimpongeze Waziri Nape Nnauye kwa juhudi zake za kuweza kumshawishi rais kukubali kuruhusu kwa timu hizo kuendelea kuutumia.
“Hivyo sasa mchezo wa kesho kati ya Azam na Simba utachezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, nitoe wito kwa mashabiki na wadau wa soka kwamba uwanja
umefungwa kamera za kisasa ambazo zitaweza kubaini matukio yote
yatakayokuwa yakijitokeza na ikukumbwe vyombo vya usalama vina mkono
mrefu, sasa ni bora tukashirikiana wote kwa pamoja kuutunza.”
Post a Comment